. Mtume salla-llaahu Alayhi wa-sallam. Alituma mtu kwa mtaalam wa hijama na akafanyiwa hijama. ( Bukhar 3.481 )
Jabir bin Abdallaah, Radhiya-llaahu anhu. Nilimckia mtume salla-llaahu Alayhi wa sallam. Akisema. kama kuna dawa ( tiba ) katka dawa zenu basi ni hijama. kunywa Asali, na chuma cha moto, lakini naukataza umma wangu kupiga chuma cha moto ( Bukhar 7.587 ) 
Abdullaah bin Abbas Radhiya llaahu anhu. Amesema mtume salla-llaahu Alayhi wa-sallam. Alifanya hijama kutibu kipanda uso wakati akiwa Ihram ( Bukhar 5701 )
Abdullaah bin Abbas pia anasimulia kuwa mtume salla-llaahu Alayhi wa-sallam. Alifanya hijama akiwa katka swaum. Bukhar 5694.
Abdullaah bin Abbas pia anasimulia kuwa mtume salla-llaahu Alayhi wa-sallam. Alifanya hijama shingoni mwake na katkati ya mabega na alimlipa tabibu wa hijama ujira wake. ( kama ingekua haraam asinge mlipa tabibu Tirmidh 49. 003/  345 ).
Anas bin Malik. Radhiya-llaahu anhu.Amesema mtume. salla-llaahu Alayhi wa-sallam. Alifanya hijama katka shingo yake na katkati ya mabega, na alipendelea kufanya tiba hii tarehe 17,   19,  21 ya miezi ya kiislaamu, ( Tirmidh 49.005./ 347 ).
Abu hurayra Radhiya-llaahu anhu. Amesema mtume salla-llaahu Alayhi wa-sallam. Amesema yeyote atakae fanya hijama tarehe 17, 19, na 21, ya miezi ya kiislaamu basi mtu huyo atajitibu kila aina ya ugonjwa " (  Abu Dawud 3861 ).